Rais Samia kuunda tume ya uchunguzi Ngorongoro

HomeKitaifa

Rais Samia kuunda tume ya uchunguzi Ngorongoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ataunda Tume mbili ambapo moja itachunguza na kutoa mapendakezo kuhusu masuala ya Ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro.

Tume nyingine itaangalia utekelezaji wa mchakato wa uhamiaji kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo Ikulu ndogo ya Arusha wakati akizungumza na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai (Malaigwanani) wanaoishi katika eneo la Ngorongoro.

Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kuwasikiliza viongozi hao kufuatia kuwepo kwa malalamiko dhidi ya baadhi ya maamuzi ya Serikali yanayohusu eneo la Ngorongoro.

Rais Dkt. Samia amesisitiza ulazima wa wananchi kushirikishwa ipasavyo katika upangaji na utekelezaji miradi inayopita kwenye maeneo yao.

Mwisho ameitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI kushughulikia changamoto zinazojitokeza ikiwemo kukosekana kwa baadhi ya huduma za msingi za kijamii katika eneo la Ngorongoro

error: Content is protected !!