Yafahamu mataifa yenye nguvu kubwa za kijeshi Afrika 

HomeElimu

Yafahamu mataifa yenye nguvu kubwa za kijeshi Afrika 

Mtandao wa Global Firepower kupitia utafiti wake umeorodhesha uwezo wa kila jeshi barani Afrika kulingana na idadi ya wanajeshi, uwezo wake wa angani, ardhini, fedha zinazotengwa kugharamia majeshi hayo, vifaa vya kijeshi, mali asili, uwezo wa majini na kadhalika.

1. Misri
Kwa jumla Misri ndilo taifa linaloongoza kijeshi barani Afrika kutokana na ukubwa wa jeshi lake. Taifa hilo limewekwa katika nambari ya 12 kote duniani.

2. Algeria
Sawa na mataifa mengine ya Afrika Magharibi, Algeria imefanikiwa katika mpaka wake mkubwa wa maji unaoipatia fursa kubwa. Taifa hilo limefanikiwa kuweka uwezo wa kijeshi ardhini, angani pamoja na majini. Hata hivyo taifa hilo linaorodheshwa la 27 kote duniani.

3. Afrika Kusini
Kwa kuwa taifa hilo halijakumbwa na mzozo wa kivita kwa muda mrefu sasa, Afrika Kusini inatumia jeshi lake lililopiga hatua kiteknolojia kuweka amani na ushirikiano wa kimataifa. Ukosefu wa mizozo haujalizuia taifa hilo kulitengea jeshi lake $4.6b.

4. Nigeria
Taifa hilo la Afrika magharibi limekuwa likikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram siku nenda siku rudi kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

5. Ethiopia
Ndilo taifa la pakee lisilo na mpaka wa majini kati ya mataifa matano bora yenye uwezo mkubwa wa kijeshi. Taifa hilo limeelekeza raslimali yake kuu kujenga jeshi lake.

6. Angola
Taifa hilo lina wanajeshi 100,000 wanaosaidiwa na magari 585 ya kijeshi, vifaru 300 ,ndege za kijeshi 285 na meli 57 za wanamaji.

7. Morocco
Mapema mwaka huu, Mfalme Mohammed VI alitoa wito kwa serikali kusajili raia 10,000 wa Morocco kuhudumia jeshini kwa lazima kwa mwaka mmoja na idadi hiyo ilitarajiwa kuongezeka hadi 15,000 kufikia mwaka 2020.

8. Sudan
Hii ni nchi iliyoleta utata katika kuingizwa kwake kwenye orodha hii mwaka huu, mashujaa waliogeuka na kuwa mabaradhuli. Baada ya maandamano ya muda mrefu na waandamanaji kuamua kukita kambi katika makao yake makuu, jeshi lilimWondoa kiongozi Omar al-Bashir aliyekuwa amehudumu kwa kipindi kirefu.

9. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni ya pili kwa idadi kubwa ya watu Afrika ambayo ni milioni 86. Umoja wa Mataifa bado una majeshi yake nchini humo kwa sababu vikosi vyake haviwezi kukabiliana na operesheni za kuleta amani kikamilifu.

10. Libya
Hakujakuwa na amani wala uthabiti katika eneo la Afrika Kaskazini tangu kung’olewa madarakani kwa Muammar Gaddafi. Libya imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tangu kuuwawa kwa rais Muammar Gadaffi.

error: Content is protected !!