Dalili 10 kuwa mwanao anatumia dawa za kulevya.

HomeElimu

Dalili 10 kuwa mwanao anatumia dawa za kulevya.

Utumiaji wa dawa za kulevya huja na dalili mbalimbali mwenye mwili wa mtu. Lakini si mara zote mtu akionesha moja ya dalili tajwa kwenye andiko hili anatumia dawa za kulevya, bali unaweza kuzitumia kama ishara kufanya uchunguzi zaidi kujiridhisha.

10. Kubadili utaratibu wa chakula
Madawa kama Heroin, Cocaine yanaweza kumuondolea mtu hamu ya kula kabisa. Matumizi ya bangi yanaweza kumfanya mtu aongezeke au apungue uzito. Bangi inawez kumfanya mtu awe anakula sana au akapunguza kabisa hamu ya kula, hivyo kupelekea kuongezeka au kupungua kwa uzito.

9. Mabadiliko ya tabia
Mabadiliko ya tabia ni moja ya dalili kubwa sana kwa watumiaji wa dawa za kulevya. Watuamiaji wa dawa za kulevya hukumbwa na hali ya mabadiliko katika utaratibu wa maisha yao ya kila siku. Watu hawa hujitenga na jamii na kuanza kukaa peke yao na hali zao hubadilika mara kwa mara, wanakuwa na hasira za karibu na wengine kuwa na tabia ya kuzungumza sana. Wengine huaza kuwa wasiri na kuanza kujihami bila sababu za msingi.

8. Mabadiliko ya ratiba ya kulala
Mtu akianza kutumia dawa za kulevya ratiba yake ya kulala lazima ibadilike. Watumiaji wa Cocaine hupata usingizi katika muda ambao si kawaida mtu kulala, na mara nyingi wanahisi kuchoka na kutamani kulala muda wote.

7. Kupoteza uwezo wa kutamka maneno kwa ufasaha
Aina nyingi za dawa za kulevya zinaweza kuathiri uwezo wa mtu wa kuongea. Mtumiaji wa dawa za kulevya huanza kupoteza uwezo wa kuongea taratibu sambamba na kutoka jasho jingi mara kwa mara na mafua yasiokwisha. Mtumiaji wa Cocaine na Bangi anaweza kupata tatizo hilo.

6. Kubadilisha marafiki kwa haraka
Mtu akianza kutumia dawa za kulevya hufanya mabadiliko ya haraka sana ya marafiki. Hupunguza uhusiano na marafiki zake wa siku zote, na mara nyingi huanzisha urafiki mpya aidha na wauzaji au wasambazaji wa dawa anazotumia. Marafiki wapya hubadili kabisa tabia zao na kuaza kufanya mambo ambayo hakuwa anayafanya awali, mambo hayo huwa yale ambayo yako kinyume kabisa na jamii yake.

5. Anapunguza kujipenda/ kujitunza
Ukiona dalili kuwa anaanza kuwa mchafu, habadilishi nguo na hata muonekano wake unabadilika kwa kuachia nywele na kuanza kutoa harufu mbaya kwenye mdomo na mwili wake, sio dalili ya kuifumbia macho. Mtu aliyeanza kutumia dawa za kulevya mara nyingi huonesha tabia hiyo, na pia kama ni mwanafunzi utaanza kuona pia anashuka kitaaluma.

4. Kutetemeka miguu na mikono
Dawa za kulevya zinaweza kumfanya mtu mtu akawa na hali ya kutetemeka mikono au miguu. Hii mara nyingi huwakuta watu wanaotumia Cocaine ambayo huathiri mfumo wa misuli kwenye mwili pamoja na kupoteza nguvu mwilini.

3. Anahitaji hela bila sababu
Kama atakuomba hela mara kwa mara na pesa hiyo haina maelezo yoyoye kuhusu matumizi yake, uwezekano ya huyo mtu kununua dawa za kulevya ni mkubwa. Mtu huyo anaweza diriki kuuza mali au vitu vyake ili akanunue dawa za kulevya. Wengine wakikosa pesa huanza tabia ya wizi.

2. Macho hubadilika kuwa mekundu
Macho hutoa maji maji na muda mwingine huvikwa na utelezi kwa juu ya mboni na kuonekana mithili ya kioo kinachong’aa. Watumiaji wa bangi, cocaine na waovuta gundi au petroli, macho yao hufifia, na mara nyingi uwezo wa kuona vizuri.

1. Usiri uliopitilizia
Ghafla utaona anaaza kujitenga na kumtenga kila mtu. Marafiki na ndugu wote wataanza kuona mabadiliko ya mtu anayetumia dawa za kulevya kwa kuanza kusema uwongo kila mara. Mtumiaji akiulizwa juu ya tabia yake huanza kupata hasira na kuondoka. Utaona uwezo wake wa kujiamini unashuka, hatoweza kukutazama machoni na anaishi kwa kujificha ficha.

error: Content is protected !!