Simu 10 ghali zaidi duniani 2021

HomeElimu

Simu 10 ghali zaidi duniani 2021

1. Falcon Supernova iPhone 6 Pink Diamond – $48.5 Milioni (111,312,000,929.46 Tsh)
Simu hii ina almasi ya pink iliyopachikwa kwa nyuma. Kampuni inayotengeneza simu hii inasema kuwa kwa wale wanaoshindwa bei ya simu hiyo, basi wameweka punguzo la bei ya dola milioni 42.5 na dola milioni 32.5 kwa simu.

2. iPhone 4s Elite Gold – $9.4 Milioni (21,798,600,182.02 Tsh)
Simu hii inatengenezwa kwa vipande zaidi 500 vya almasi vinavyoizunguka simu hiyo. Simu hii maalumu kwa watu maalumu, zimetengenezwa mbili tu duniani.

3. iPhone 4 Diamond Rose Edition – $8 Million (18,552,000,154.91 Tsh)
Hii imezungushiwa vipande zaidi ya 500 vya almasi. Halafu kuna vipande 53 vya almasi kwenye nembo/logo ya Apple . Duniani ziko mbili tu.

4. Goldstriker iPhone 3GS Supreme – $3.2 Million (7,420,800,061.96 Tsh)
Hii imezungushiwa vipande 36 vya almasi na nyongeza ya vipande vingine 71 vya almasi vyenye karati 22 za dhahabu. Imechukua miezi kumi kuitengeneza.

5. iPhone 3G Kings Button – $2.5 Million (5,797,500,048.41 Tsh)
Simu hii kitufe chake cha katikati ni dhahabu ngumu ya njano yenye mchanganyiko wa dhahabu nyeupe. Upande wa pembeni umezungushiwa na vipande 138 vya almasi. Kitufe cha katikati licha ya  kuwa na dhahabu, lakini pia kina nakishi za almasi.

6. Diamond Crypto Smartphone – $1.3 Million ( 3,014,700,025.17 Tsh)
Inatajwa kuwa simu salama zaidi duniani dhidi ya wadukuzi. Pembe za simu hii ni almasi tupu.

7. Goldvish Le Million – $1 Million (2,319,000,019.36 Tsh)
Simu hii ilitengenezwa mwaka 2006 na kampuni ya Sweden inayoitwa Goldvish mwaka . Simu hii ilikuwa na camera yenye MP 2.6 na resolution ya 1600 x 1200. Simu hii ina dhahabu nyeupe na ya njano.

8. Gresso Luxor Las Vegas Jackpot – $1 Million (2,319,000,019. Tsh)
Simu hii kwa jinsi ilivyo hali zimetengenezwa 3 tu duniani. Imetengenezwa kwa gramu 180 za dhahabu na almasi nyeusi.

9. Goldvish Revolution – $488,150 (1,132,019,859.45 Tsh)
Simu hii ina vipande 29 vya almasi, vipande 18 vya almasi na vipande vya dhahabu nyeupe ambayo ipo kwa kiasi kikubwa kwenye simu hiyo. Betri yake imetengenezwa kwa Lithium, kioo chake ni inchi 2.2. Imewekwa lugha kama kiarabu, kiingereza, kirusi, kifaransa, kijerumani na kireno.

10. Virtue Signature Cobra – $310,000 (718,890,006.00 Tsh)
Simu hii imetengenezwa na kampuni ya Kifaransa ya Boucheron. Simu hii ni muunganiko wa vipande/sehemu 388 ambazo zimeunganishwa nchini Uingereza. Kioo chake ni HD chenye ukubwa wa inchi 5.2 na uwezo kuhifadhi data wa 64 GB. Camera yake ni MP 21 na ina uwezo wa 4G LTE, 3G, Wi-Fi, GPS and NFC.

 

 

error: Content is protected !!