Barua ya wazi ya Mpambazi kwenda kwa Kigogo

HomeMakala

Barua ya wazi ya Mpambazi kwenda kwa Kigogo

Mwandishi Andrew Mpambazi.

Sina shaka ya kuanza kujitambulisha kwa kuwa wanifahamu. Nachukua muda huu kukuandikia yafuatayo tafadhali naomba soma barua yangu.

Waswahili walisema hakuna mwalimu mkali kama ulimwengu maana yeye hana huruma, hana maswali wala majibu. Nae ulimwengu huishi kati yetu nikiwa na maana ya kwamba funzo ulilonipa japo kwa ukali limenijenga na kunifanya niwe vizuri na mitaa kwa maana ilipaswa niyapitie haya ili yanijenge imara zaidi.

Nashukuru sana sana kwa funzo maana naamini Mungu alikuleta uwe mwalimu mzuri katika kusahihisha makosa yaliokuwepo katika biashara yangu.

Sasa basi nakusihi tusameheane tusahau yote yaliyopita na tugange yajayo kama Mt. Paulo alivyotuagiza katika kitabu cha Waefeso 4:31-32;

“Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.”

Hivyo basi naamini tunaenda kufungua ukurasa mpya na kusahau yote yalitokea pia napenda nikukumbushe kuwa mimi ni mjasiriamali mdogo ambae kesho yangu naiandaa leo najituma huku kwenye ujasiriamali kwa kuwa nyumbani hakuna cha kurithi bali nina majukumu ya kuwatunza wazazi wangu.

Kwa kusema hayo naomba nikushukuru tena kwa muda wako na kuanza ukurusa wetu mpya kwa sala hii fupi “Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.

COMMENTS

error: Content is protected !!