Naomba radhi : Spika Ndugai

HomeKitaifa

Naomba radhi : Spika Ndugai

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewaomba radhi Wakristo na Watanzania wote kufuatia kauli aliyoitoa Bungeni leo.

Katika kauli zake wakati akiongelea adhabu iliyotolewa kwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, Spika Ndugai alijikita katika mistari ya Biblia, ambapo alisema “Yesu alitembea na mke wake kutoka Nazareti…”

Spika Ndugai amesema hapo ulimi wake uliteleza katika hali ya kibinaadamu, alichotaka kusema ni kwamba “Yusufu alitembea na mke wake kutoka Nazareti..”

error: Content is protected !!