Mfahamu Dkt Tax, mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa ulinzi Tanzania.

HomeMakala

Mfahamu Dkt Tax, mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa ulinzi Tanzania.

Historia mpya imeandikwa leo nchini Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania imepata Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye ni mwanamke. Huyu ni Dkt Stergomena Tax.

Dkt Stergomena Tax ni nani?

Ni mzaliwa wa Magu mkoani Mwanza. Alizaliwa Julai 6, 1960.

Alipata elimu ya sekondari katika shule moja na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Shule ya Sekondari Lake ya huko Mwanza.

Alipata shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kabla ya kwenda kazi za juu zaidi nje ya nchi alikobobea katika masuala ya maendeleo ya kimataifa.

Dkt. Tax amewahi kuitumikia nchi katika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uhusiano wa Afrika Mshariki (2008-2013).

Mwaka 2013 katika mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Tax aliteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo. Amedumu katika nafasi hiyo hadi mwezi Agosti 2021 alipomaliza muda wake.

Septemba 10, 2021 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Dkt Tax kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Septemba 12 alimteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na sasa ameaapa kutumikia nchi katika nafsi hiyo.

error: Content is protected !!