Rais Samia: Mabadiliko serikalini yanaendelea

HomeKitaifa

Rais Samia: Mabadiliko serikalini yanaendelea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kufanya mabadiliko katika nafasi mbalimbali ndani ya serikali yake.

Akihutubia baada ya kuwaapisha mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliowateua jana, Rais Samia amesema baada ya kutumia miezi 6 ya kutazama mwenendo wa watendaji mbalimbali wa Serikali, anaona haja ya kufanya mabadadiliko.

“Kipindi cha miezi 6 nilikuwa najifunza, nimeona sasa vipi nakwenda na nyie, nami nimejichagulia njia yangu, nataka niwaambie kuwa tunakoelekea huko Serikali yetu itaendeshwa kwa matendo. makali na sio maneno makali. Ninaposema matendo makali sio kupigana mikwaju, ni kwenda kwa wananchi na kutoa huduma inayotakiwa,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, ameongeza,“Wizara moja katika Wizara ambazo nimezipangua portfolio, ilitakiwa uongozi wake uwepo hapa uape hapa uape upya. Lakini kama nilivyosema hapa nilipofika nimewekwa koma sikuweka ‘full stop’,.. Wizara hii nayo tutaifanyia marekebisho watakuja kuapa mbele yenu.”

Mwishoni mwa hotuba yake pia, Rais Samia aliwaaga viongozi waliofika Ikulu na kusema kwamba yeye anaendelea na kazi ya kufanya mabadiliko.

error: Content is protected !!