Orodha ya magari 6 ghali zaidi duniani kwa sasa

HomeBurudani

Orodha ya magari 6 ghali zaidi duniani kwa sasa

Kumiliki gari zuri, yawezekana ni ndoto ya kila mtu duniani, pamoja na mambo mengine kama nyumba, ardhi, kazi na vitu vingine vya thamani.

Wasanii, wanamichezo na watu wengine maarufu dunaini mara nyingi hutumia magari ya kifahari zaidi na yenye thamani kubwa kwa sababu ya shughuli zao na namna wanavyojiweka kwenye macho ya watu wanaowafuatilia.

Ifuatayo ni orodha sita ghali zaidi duniani kwa mujibu wa mitandao mikubwa kama Luxe.digital, motor 1 na wealthygorilla.

6: Mercedes-Maybach Exelero – $8.0 milioni

The Maybach Exelero – Maybach

Gari moja la Maybach Exelero linagharimu dola milioni 8 na linaweza kwenda kwa mwendo wa kasi wa juu zaidi wa kilometa 351 kwa saa. Gari hili limetoka toleo moja tu na linamilikiwa na Dr. Andre Action Diakite Jackson.

Matairi ya gari hii yana ukubwa wa inchi 21 yakitajwa kuwa ya kipekee katika aina ya magari yanayofanana na haya ya ‘sports cars’. Lina uwezo wa kubeba uzito wa mpaka kilo 2,721.

Pamoja na uzuri wake, Mercedes ilitangaza kutozalisha tena aina hii ya magari na kujielekeza zaidi kwenye magari mengine ya kifahari ya S-Class.

5. Bugatti Centodieci – $9.0 milioni

Bugatti Centodieci - Wikipedia
Moja ya magari yenye nguvu zaidi duniani ikiwa na horsepower 1,600. Ikileta historia yenye asili ya ufaransa, si nguvu tu bali hata thamani yake haishikiki, linauzwa kati ya $8.9 na $9.0 milioni.

Gari hili lina uwezo wa kwenda mwendo wa kilometa 379 kwa saa.

4. Rolls-Royce Sweptail – $13milioni

10 Things You Didn't Know About the Rolls Royce Sweptail

Rolls-Royce Sweptail ni toleo lenye thamani zaidi katika jamii ya magari ya Rolls-Royce. Ghari hili lililotengenezwa Uingereza lilitoka kama toleo la kipekee mwaka 2013 lakini sasa sokoni linatajwa kugharimu dola milioni $13.

Gari hilo linatajwa kuwa ndilo linaloiweka Uingereza kwenye ramani ya nchi zenye magari ya kifahari, yenye muundo unaovutia na nguvu ya horsepower 453.

3. Pagani Zonda HP Barchetta – $17 Milioni

LCD Models New Pagani Zonda HP Barchetta! (UPDATE) • DiecastSociety.com

Zonda HP Barchetta lilikuwa toleo lake la mwisho lililokuwa na kipekee kabisa. Italia gari hili linaitwa ‘boti ndogo’ kwa namna muundo wake ulivyo na uwezo wake wa kupita sehemu mbalimbali licha ya kuonekana ni gari ‘mayai’.

Gari hili lina kasi ya kilometa 355 kwa saa. Magari haya yalitengenezwa matatu tu na gari ya mwisho liliuzwa kwa dola milioni $17.6 na kufanya kuwa moja ya magari yenye thamani zaidi duniani.

2: Bugatti La Voiture Noire – $18.7 Milioni

Bugatti La Voiture Noire Final Version: This Is The $13.4M Hypercar
Gari hili ambalo limefanana na Jean Bugatti ya mwaka 1934, ni gari linalovutia sana na kufanya kuwa moja ya magari ya bei ya juu kabisa kuwahi kuuzwa. Limeuzwa kwa dola $19 millioni. Lina horsepower 1500 na mwendo kasi wa kilometa 420 kwa saa.

Kwa kukadiria tu thamani ya gari moja la Bugatti La Voiture Noire unaweza kujenga karibu nyumba 400 za kiwango cha kati zenye vyumba vinne na kila kitu ndani. Ukithaminisha nyumba hiyo kwa thamani ya dola 45,000 mpaka 55,000 kwa moja.

1: Rolls-Royce Boat Tail – $28.0 Milioni

Rolls-Royce Boat Tail Revives The Art Of Coachbuilding
Ni toleo la kipekee ambalo kwa miaka minne limekuwa likitengenezwa muondo na muonekano wake. Ukilitaka gari hili lenye friji mbili ndani litatengenezwa kwa mahitaji yako yakiwemo ya rangi.

Ingawa haijathibitishwa, inaelezwa kuwa Jay Z na mkewe Beyonce ndio walioweka oda ya kutengenezewa gari hili. Lakini taarifa rasmi ni kwamba yatatengenezwa magari matatu tu ya Rolls-Royce Boat Tail 2021 na moja litauzwa kwa dola $28.0 Million.

 

error: Content is protected !!