Usiyoyajua kuhusu Dkt Ashatu Kijaji, Waziri mpya wa habari

HomeMakala

Usiyoyajua kuhusu Dkt Ashatu Kijaji, Waziri mpya wa habari

Dkt Ashatu Kijaji ameapishwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Tumekuwekea baadhi ya taarifa zinazohusu safari ya Dkt. Kijaji Hususan katika uongozi.

Alizaliwa Aprili 26, 1976.

Alipata elimu ya sekondari huko mkoani Shinyanga katika Shule ya Shycom kabla kujiunga na Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro na kuhitimu mwaka 2001. Alirudi tena Mzumbe kama mhadhiri na mwaka 2008 alipata shahada uzamili.

Mwaka 2013 alipata shahada ya uzamivu kutoka chuo kikuu cha Agder nchini Norway.

Jina lake katika siasa,lilivuma zaidi mwaka 2015 aliposhinda Ubunge wa jimbo la Kondoa Vijijini mkoani Singida baada ya kuchuana vikali  na Yasi Shaban wa Chama cha Wananchi-CUF.

Mwaka 2015 Dkt. Kijaju aliteuliwa kuwa Naibu wa Waziri wa Fedha na Mipango.

Mwaka 2020 alishinda tena Ubunge huko Kondoa Vijijini.

Hivi sasa Dkt. Kijaji ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

error: Content is protected !!