Njia za kuwa mwanasiasa mwenye mafanikio

HomeKitaifa

Njia za kuwa mwanasiasa mwenye mafanikio

1.Shiriki katika mipango na shughuli za jamii.

Kabla ya kugombea nafasi yoyote katika serikali, utahitaji kushiriki katika nafasi za chini za siasa mpaka kufikia nafasi za juu. Ili kuwa na ufanisi katika kiwango cha eneo lako, unahitaji kuungana na jamii yako na kushirikiana nayo. Unapaswa kujitolea kwa jamii ili kujua mahitaji na changamoto wanazopitia.

2.Tengeneza uwepo wako katika jamii

Tumia wakati wako kujitolea kushiriki katika shughuli mbalimbali za jamii inayokuzunguka kwa kuionesha jamii yako kuwa uko tayari kujitolea nguvu zako kwa kuhitaji kufanya mema, sio mpaka ulipwe. Hii itakua na faida baadaye unapoamua kugombea.

3.Ungana na viongozi wa jamii.

Unapaswa kuwasiliana na viongozi katika jamii yako na kuungana nao. Hii itasaidia kuweka msingi wa kampeni yako baadaye, Huu ni mtaji wako utakaoutegemea wakati utakapofika. Uhusiano thabiti na viongozi hawa pia utakuruhusu kujifunza na kuangalia jinsi viongozi hawa wanavyojiendesha katika jamii.

4.Changia maoni yako katika mikutano na midahalo ya ndani.

Unapaswa kutumia mikutano kama fursa ya kutumia ujuzi wako wa kuzungumza hadharani, hata kama sio mikutano ya kisiasa. Jaribu kuwa machoni pa umma iwezekanavyo, haswa kwa sababu ambazo unapenda sana. Unapaswa pia kushiriki katika mijadala kama mwakilishi wa jamii yako, kwani hii itakuruhusu kuonyesha shauku yako ya mabadiliko na uwezo wako wa kuzungumza hadharani.

Mbali na kuzungumza na hadhira kubwa, unapaswa pia kuwa na tabia ya kuongea na watu binafsi katika jamii moja kwa moja. Kufanya hivi utazoea kuwasiliana na watu kwa kiwango kikubwa na kutengeneza uhusiano binafsi na wapiga kura wako watarajiwa.

error: Content is protected !!