Rais Samia apewa kongole na mabalozi

HomeKitaifa

Rais Samia apewa kongole na mabalozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amepokea hati za utambulisho wa mabalozi watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam ni Martin Klepetko (Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini), Maria Alejandra (Balozi wa Jamhuri ya Chile hapa nchini), Pavel Vziatkin (Balozi wa Jamhuri ya Belarus hapa nchini).

Wengine ni Luke Joseph Williams (Balozi wa Australia hapa nchini) na Monica Greiff Lindo (Balozi wa Jamhuri ya Colombia hapa nchini). Mabalozi hao wote makazi yao ni Jijini Nairobi nchini Kenya.

Akizungumza mara baada ya kupokea hati hizo, Rais Samia amewapongeza mabalozi hao na kuwaomba kufikisha salamu zake kwa viongozi wakuu wa nchi hizo na kusisitiza kuwa Tanzania ipo tayari kuendeleza uhusiano na ushirikiano kwa manufaa ya pande zote.

Kwa upande wao, mabalozi hao wamempongeza kwa utendaji mzuri na kumuahidi ushirikiano Rais Samia.

COMMENTS

error: Content is protected !!