Zelensky: Naomba kuhutubia Muungano wa Afrika

HomeKimataifa

Zelensky: Naomba kuhutubia Muungano wa Afrika

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa ombi jipya la kutaka ahutubie wakuu wa mataifa ya Muungano wa Afrika (AU), kulingana na Kamishna wa AU, Moussa Faki.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Bw Faki alisema alipokea ombi wakati wa mazungumzo ya simu na Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine.

Wawili hao walizungumza kuhusu Rais Zelensky “kutaka kuendeleza uhusiano wa karibu na AU”.

Mapema mwezi huu, Rais Zelensky alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Senegal Macky Sall, ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa AU, na akamuomba ahutubie viongozi wa Afrika.

Azimio hilo liliidhinishwa kwa kura 93, 24 zipalipinga na 58 ziliepuka kupiga kura.

error: Content is protected !!