Mo Salah aibuka mchezaji bora

HomeMichezo

Mo Salah aibuka mchezaji bora

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah amechaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Soka kwa 2021/22.

Salah, 29, amechangia mabao 22 na asisti 13 katika michezo 31 pekee ya Ligi Kuu ya Uingereza na kukisaidia kikosi hicho cha Jurgen Klopp kushika nafasi ya pili kwenye jedwali, pointi moja nyuma ya mabingwa Man City zikiwa zimesalia mechi tano pekee msimu huu.

Kwa  jumla, Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri amehusika katika mabao 30 na pasi 14 za mabao katika mechi 44 pekee za michuano yote, ni kiwango bora ambacho hadi sasa kimeisaidia Liverpool kushinda Kombe la Ligi, na kutinga fainali ya Kombe la FA na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Salah, ambaye alimrithi mshindi wa mwaka jana, beki wa City, Ruben Dias, pia ndiye mfungaji bora wa sasa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuzifumania nyavu mara 22, tano zaidi ya Heung-Min Son na Cristiano Ronaldo, huku fowadi huyo akiwa ndiye anayeongoza kwa kutoa pasi za mabao.

 

error: Content is protected !!