Tulia aonya mawaziri teuzi za mabalozi

HomeKitaifa

Tulia aonya mawaziri teuzi za mabalozi

Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amewasihi mawaziri kuzingatia vigezo pindi wanapochagua mabalozi wa wizara zao, na sio kuwachagua kwa sababu ya kufahamiana.

“Waheshimiwa mawaziri mnapoteua mabalozi muwe na vigezo mahususi vinavyojulikana ambavyo akitajwa mtu fulani itajulikana kabisa yule anazo sufa hizo ambazo mwingine hana, kwahiyo hizi nafasi za ubalozi kwa sababu sio ubalozi kama anaoteua mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anamteua ampendaye , nyinyi upande serikali mnavyowateua hawa mabalozi msiteue muwapendao mteue wenye vigezo,” alisema Spika Tulia.

Amezungumza hayo leo Bungeni baada ya Mbunge wa Viti maalum, Agnesta Lambert kuhoji kuhusu kuteuliwa kwa mabalozi katika sekta mbalimbali.

error: Content is protected !!