Rais Samia mgeni rasmi maonesho ya teknolojia ya madini

HomeKitaifa

Rais Samia mgeni rasmi maonesho ya teknolojia ya madini

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yatakayofanyika mkoani Geita kuanzia tarehe 20 hadi 30 Septemba, 2023 katika Uwanja wa EPZ-Bombambili.

Ufunguzi wa maonesho hayo utafanyika tarehe 23 Septemba na kufunguliwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko huku Mgeni Rasmi akiwa Rais Samia Septemba 30 2023.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira”.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita kwa kushirikiana na TANTRADE na Halmashauri ya Mji Geita imesema kila mtu anakaribishwa kwenye maonesho haya na hakuna kiingilio chochote hivyo wananchi au wenye vyombo vya usafiri wanakaribishwa.

error: Content is protected !!