Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 05 (Ranieri rasmi Watford, Sanchez njia panda Inter Milan)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 05 (Ranieri rasmi Watford, Sanchez njia panda Inter Milan)

Mmiliki wa Newcastle United, Mike Ashley anajua njia pekee ya kumbadili kocha mkuu wa Newcastle ni kulipa kila kandarasi ya Steve Bruce ambayo alikubali mnamo Julai 2019 (Chronicle Live).

Claudio Ranieri (69) ametia saini kuwa kocha mkuu mpya wa Watford baada ya kuondoka kwa Xisco Munoz siku ya Jumapili (Sky Sports).

Mshambuliaji wa Uholanzi anayecheza Bayern Munich Joshua Zirkzee 20, anasema alikataa nafasi ya kujiunga na Everton mwaka 2017 (Het Nieuwsblad via Liverpool Echo).

Manchester City wanamfuatilia kiungo wa kati wa Uhispania Nico Gonzalez anayekipiga Barcelona, ambaye hajapewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza (Fichajes – Spanish).

        > Fahamu kwanini Facebook, Instagram na Whatsapp zilitoweka hewani

Beki wa Ujerumani anayekipiga kunako klabu ya Borussia Monchengladbach, Luca Netz anadai alikataa uhamisho aliosema “hauna maana’’ kwenda Manchester City miaka mitatu iliyopita, mchezaji huyo mwenye miaka 18 anasema atawakatalia kwa mara nyingine tena (Sun).

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Alexis Sanchez (34) hajui mustakabali wake na klabu ya Inter Milan baada ya mchezaji huyo kuchapisha kisha kufuta ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter uliokuwa ukikosoa kitendo cha kukosa muda wa kucheza uwanjani (Mirror).

Beki, raia wa Ivory Coast Serge Aurier 28, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Tottenham Hotspurs, anajiandaa kujiunga na Villarreal ya Uhispania (L’Equipe – in French).

Aliyekuwa kiungo wa kati Manchester City, Yaya Toure 38, ametoa ofa kwa Barcelona wakati huu wakiwa katika changamoto, lakini haijulikani kama anataka kucheza au kufundisha (Sun).

error: Content is protected !!