Maendeleo ujenzi Daraja la JPM yamridhisha Kinana

HomeKitaifa

Maendeleo ujenzi Daraja la JPM yamridhisha Kinana

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Magufuli lililopo maeneo ya Kigongo Busisi mkoani Mwanza

Daraja hilo linalounganisha mikoa ya Mwanza na Geita ujenzi wake umefikia asilimia 51 na linatarajiwa kukamilika Februari mwaka 2024.

Akizungumza mara baada ya kukagua daraja hilo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amesema chama kinaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wake na ana imani utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa, hivyo mwaka 2024 nchi itakuwa imepata alama kubwa ya kuwa na daraja refu kuliko yote Afrika Mashariki likiwa na urefu wa kilomita 3.2.

“Najaribu kukumbuka madaraja mangapi Afrika yenye urefu huo kama hili halitukua la kwanza basi litakuwa katika tatu bora.

“Hivyo niwapongeze wote wanaoshiriki ujenzi wa daraja hili ndugu zetu wa kutoka Korea, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wajenzi kutoka Kampuni ya China na Watanzania wote wanaoshiriki,” amesema Kinana.

error: Content is protected !!