Kivuko kipya Kigamboni

HomeUncategorized

Kivuko kipya Kigamboni

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa ameeleza kufurahishwa na hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelekeza kununuliwa kwa kivuko kipya kwa ajili ya wanaosafiri kutoka na kuingia wilayani humo.

Nyangasa ameyasema hayo leo, Novemba 11, 2022 alipotoa salamu za Wilaya hiyo katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Kigamboni.

“Hatua ya maelekezo yako kwa ajili ya kununua kivuko kipya kikubwa kuliko vyote vilivyopo sasa nikushukuru sana, sisi wana Kigamboni tunasubiri kwa hamu kupatikana kwa kivuko kipya ili kazi iendelee zaidi,” amesema.

error: Content is protected !!