Mpango kumuwakilisha Rais Samia Rwanda

HomeKitaifa

Mpango kumuwakilisha Rais Samia Rwanda

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 05 Septemba 2022 amewasili Kigali nchini Rwanda ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika wa Mwaka 2022 (AGRF 2022).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mheshimiwa Vincent Biruta .

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 6 hadi 9 Septemba 2022 ukiwa na lengo la kujadili Hatua Madhubuti kwaajili ya Mifumo ya Chakula inayostahimili. Mkutano wa AGRF 2022 unashirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kimataifa pamoja na Wadau wa Kilimo.

error: Content is protected !!