Apple yaondoa Application ya Quraan kwenye simu zake

HomeKimataifa

Apple yaondoa Application ya Quraan kwenye simu zake

Kampuni ya Apple, watengenezaji wa simu za iPhone imeondoka programu tumizi “app” ya ‘Quran Majeed’ kwenye simu za iPhone zinazotumika nchini China. Apple imechukua uamuzi huo kufuatia agizo la Serikali ya China.

‘Application’ hiyo iitwayo ‘Quran Majeed’ in mamilioni ya watumiaji duniani. BBC imeripoti kwamba programu hiyo imendolewa kwa sababu inatoa jumbe ambazo zinavunja sheria za China, licha ya kwamba Serikali ya China haijatoa tamko hadi hivi sasa, na bado haijulikana hasa chanzo cha China kuagizwa kuondolewa kwa programu hiyo.

Kuondolewa kwa programu hizo kwenye soko la China, iligunduliwa na tovuti ya ‘Apple Censorship’ ambayo kazi yake ni kufuatilia ufanisi na utendaji kazi wa programu mbalimbali mtandaoni. Kampuni inayomiliki programu hiyo ya Quran, PDMS imesema kuwa, “Kwa mujibu wa Apple, programu hiyo imeondolewa kwa watumiaji wa Apple China kwa sababu ina maudhui ambayo yanahitaji kuwasilishiwa nyaraka zaidi za maelezo kwa Serikali ya China, bado tunajaribu kuwasiliana na Serikali ya China kuona namna ya kusuluhisha mgogoro huu.”

Programu hiyo ina watumiaji takribani milioni moja nchini China, na watumiaji milioni 35 duniani kote.

Ingawa Chama cha Kikomunist kinachoongoza Serikali ya China kinaitambua dini ya Kiislamu lakini nchi hiyo imekuwa ikiandamwa sana kwa uvunjifu wa haki za Binadamu hasa kwenye mauaji ya Waislamu wa jamii ya Uyghur.

China ni moja ya eneo ambalo kampuni ya Apple inalitegemea sana kwa soko, usambazaji pamoja na uzalishaji wa vifaa mbalimbali kutokana na idadi kubwa ya watu na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

error: Content is protected !!