Rais Samia kufanikisha ujenzi wa jengo la tiba ya mionzi KCMC

HomeKitaifa

Rais Samia kufanikisha ujenzi wa jengo la tiba ya mionzi KCMC

Katika sherehe za Jubilei ya miaka 50 ya Hospitali ya KCMC, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amesema Serikali itasimamia utekelezaji wa ahadi yake ya kughramia kwa asilimia 100 ujenzi wa jengo la utoaji tiba kwa njia ya mionzi ambalo litagharimu pesa za Kitanzania bilioni 4, na tayari wameshatoa bilioni moja huku bilioni Moja ikitarajiwa kutolewa karibuni.

Rais Samia ameeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na KCMC kuhakikisha huduma za afya zinasogezwa karibu zaidi na wananchi, kwani tayari kupitia hospitali ya KCMC tayari kuna mtambo mkubwa wa kuzalisha hewa tiba yaani oksijeni ambao kwa siku unazalisha mitungi mia 400 na kuchangia kupunguza tatizo la hewa tiba katika kanda ya Kaskazini hususani katika mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Rais pia ameipongeza KCMC kwa kuwa na huduma mbalimbali za kibingwa zinazochochea kuwepo kwa utalii tiba nchini kwani watu wanatoka nchi jirani na kuja kutibu Tanzania. KCMC pia inatarajia kuanzisha kitengo cha huduma za moyo ambapo itasaidia kupunguza wagonjwa katika hospitali ya kitengo cha wagonjwa wa moyo cha Jakaya Kikwete.

Jengo hilo la tiba mionzi litakapokamilika litasaidia kuhudumia watu wenye kansa na kuokoa maisha ya watu wengi hapa nchini.

error: Content is protected !!