Mitandao ya kijamii yazimwa Swaziland

HomeKimataifa

Mitandao ya kijamii yazimwa Swaziland

Serikali ya jamii ya watu wa Swazi chini ya mfalme Mswati wa III imelalamikiwa kwa kuzima mtandao nchini humo ili kuzuia watumiaji wa mitandao ya kijamii kuendelea kusambaza picha na video zinazoonesha waandamanaji wakishambuliwa na Jeshi la Polisi pamoja na watoto wadogo wa shule wakiwa wamejeruhiwa na Polisi.

Hii ni mara ya pili kuzimwa kwa mtandao nchini humo ambapo mara ya kwanza mtandao ulizimwa Juni na Julai kwa muda wa wiki baada ya kuwepo kwa maandamano yaliopelekea vifo vya watu 28.

Msemaji wa Mtandao wa Mshikamano wa jamii ya Uswazi (Swaziland Solidarity Network) Lucky Lukhele alishutumu hatua ya serikali na kumuelezea Mfalme Mswati III kama “mshenzi.”

“Watu wengi wamekufa, mfalme ametenda uhalifu dhidi ya ubinadamu na anastahili kuwa katika mahabusu za mahakama ya uhalifu ya Kimataifa. Anastahili kushtakiwa kwa mauaji ya zaidi ya Waswazi 200. Umoja wa Mataifa ulipaswa kumkamata mfalme huyu wa kinyama kwa kuua watoto hawa wasio na hatia.” Ameeleza Lukhele

Inaelezwa kuwa katika kufanikisha hayo yote Mfalme Mswati III anasaidiwa na binti yake ambaye anahusika na kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano nchini humo pamoja na kampuni kutoka Afrika kusini inayojulikana kama MTN.

error: Content is protected !!