Watu bilioni 3 wanakosa lishe bora duniani

HomeKimataifa

Watu bilioni 3 wanakosa lishe bora duniani

Katika ujumbe wake wa siku ya leoa ambayo ni siku ya chakula duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amesema siku hii siyo tu ni kumbusho la umuhimu wa chakula kwa kila mtu duniani, bali pia ni wito wa kuchukua hatua ili kufikia uhakika wa chakula kote duniani.

“Leo hii karibu asilimia 40 sawa na watu bilioni 3 hawawezi kumudu lishe bora, njaa inaongezeka, sanjari na utapiamlo na utipwatipwa.”

Amesema kuwa athari za kiuchumi za janga la Corona (UVIKO-19) imesababisha hali ya chakula kuwa mbaya zaidi kwani limewaacha watu wengine zaidi milioni 140 wakikosa fursa ya chakula wanachokihitaji.

“Jinsi watu wanavyozalisha, kutumia na kutupa chakula kunaathiri vibaya dunia yetu. Kunaongeza shinikizo kwa maliasili yetu, hali ya hewa na mazingira na hivyo kutugharimu matrilioni ya dola kila mwaka.” amesema Gutterres.

Katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani Guterres amesitiza kila mtu kujiunga na jumuiya ya kimataifa katika kuchukua hatua za mabadiliko na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu kupitia mifumo ya chakula ambayo itazalisha lishe bora, mazingira bora na maisha bora kwa kila mtu.

error: Content is protected !!