Mwanafunzi wa darasa la 6 amuua mwenzake kisa ugali

HomeKimataifa

Mwanafunzi wa darasa la 6 amuua mwenzake kisa ugali

Polisi kwenye kaunti ya Kakamega nchini Kenya wanamshikilia mwanafunzi wa darasa la Sita mwenye umri wa  miaka 14 anayeshutumiwa kumuua mwenzake kwa kumpiga na kitu kizito na kisha kumtupa mtoni kisa chakula cha ugali na kunde.

Mauaji hayo yametokea siku ya Alhamisi baada ya Mwanafunzi huyo kurudi kutoka shule, alipoulizia chakula akaambiwa kwamba jirani yake ambaye ni Mwanafunzi mwenzake  mwenye miaka 10 amekula ndipo alipoamua kumfuata na kumpiga na kitu kizito kichwani.

Imeripotiwa kwamba siku iliyofuata mtuhumiwa alienda shule na kuwaeleza kwamba amemuua mwenzake na kumtupa mtoni, walimu walitoa taarifa polisi na kwenda mpaka mtoni kuchukua mwili wa marehemu ulikua umejeruiwa vibaya kichwani.

Polisi wamesema kwamba mwili wa marehemu umepelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya Kakamega huku upelelezi mwingine ukiendelea.

error: Content is protected !!