Amuua mume wake kwa kumkaba usingizini

HomeKitaifa

Amuua mume wake kwa kumkaba usingizini

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Maria Matheo, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kumuua mume wake, Gabriel Nguwa (80) kwa kumkaba shingoni akiwa amelala.

Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao zinasema kuwa tukio hilo limetokea Mei 30 mwaka huu  majira ya saa nane usiku katika kitongoji cha Bugwed, Kijiji cha Budushi, Kata ya Budushi wilayani Nzega mkoani Tabora.

Akieleza chanzo cha mauaji hayo, Kamanda Abwao alisema wanandoa hao walikua na mgogoro wa muda mrefu hususani nyakati za jioni, mke anapolewa huwa anamtuhumu mumewe kuwa hakuwa na msaa wowote katika maisha yao.

Kamanda Abwao alisema kwamba mbinu iliyotumika ni kumvizia mume akiwa amelala na kumkaba shingoni na kumsababishia kifo. 

error: Content is protected !!