Miriam Odemba aziwaza tuzo za BASATA

HomeBurudani

Miriam Odemba aziwaza tuzo za BASATA

Mwanamitindo maarufu nchini, Miriam Odemba amejiunga rasmi na tasnia ya muziki ambapo katika siku ya kusherekea kumbukizi yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 40 aliachia ngoma yake ya kwanza unaoitwa ‘Rafiki” na kuasema kwamba anaamini atachukua tuzo tatu za Tanzania.

Miriam alisema kwamba kutokana na maudhui ya kazi yake mpya anaamini kuchukua tuzo tatu katika vipingele vya Msanii bora wa kike, msanii bora wa mwaka na video bora ya mwaka.

“Msanii yoyote anayejiamini anipe mkono tushindane, nipe mkono tushindane. Huu ndio wimbo bora wa mwaka, naamini zile tuzo za BASATA na kwarua tatu,” alisema Miriam.

Miriamu ambaye aliwahi kuwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania mwaka 1998, huku akishika nafasi nyingine katika mashindano ya urembo wa Dunia, katika wimbo huo ameungana na kikundi cha watoto wasiojiweza cha Matumaini Center Children na Sauti From East.

error: Content is protected !!