Reli ya kisasa kuanza kutumika rasmi Aprili

HomeKitaifa

Reli ya kisasa kuanza kutumika rasmi Aprili

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewataka viongozi wa Shirika la Reli nchini (TRC) kuhakikisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa kilometa 300 kinakamilika na kuanza majaribio ya awali mwishoni mwa Aprili.

“Ifikapo mwisho wa mwezi ujao nataka kazi ya ujenzi wa sehemu hii iwe imekamilika na treni ya majaribio ianze kazi,” alisisitiza Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa alizungumzia umuhimu wa kuweka mifumo ya kisasa ya kieletroniki katika kukata tiketi na kupata wapangaji watakaotoa huduma bora na za kisasa katika stesheni zote za reli hiyo.

Endapo ujenzi wa reli hiyo utakamilka, utapunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na msongamoano wa magari na kupunguza uchafuzi wa mazingira kwani reli hiyo itatumia umeme na hivyo haitazalisha kaboni.

error: Content is protected !!