Vijana 853 waliofukuzwa waruhusiwa kurudi kwenye Makambi ya JKT

HomeKitaifa

Vijana 853 waliofukuzwa waruhusiwa kurudi kwenye Makambi ya JKT

Vijana 854 kati ya 24000 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliofukuzwa na kusimamishwa mafunzo mwaka 2021 kwa kosa la vitendo vya uhasi wamesamehewa na kuamuriwa kurudi jeshini ili kuendelea na kazi.

Taarifa hii imetolewa na Luteni Kanali Gaudentius Grevas Ilonda, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusoano (JWTZ).

Mnamo April 12,2021 kuna Vijana wetu wa Kitanzania ambao walikuwa wanaendeea na mafunzo yao kwenye Makambi ya JKT, Vijana hao walikuwa 854 walikuwa wanendelea na mafunzo kwa kujitolea, wote walifukuzwa na kuondolewa makambini na walirejeshwa majumbani mwao kutokana na sababu za kimakosa ya kinidhamu,” 

“Baada ya Vijana hao kufukuzwa wakawa wameondolewa makambini, JWTZ imepokea na ina taarifa Kijana mmoja kati ya wale Vijana 854 amefariki na walio hai ni Vijana 853,”

“Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa kwa Umma wa Watanzania kwamba Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo ametoa msamaha kwa Vijana wote 853 na ametoa maelekezo na ameamuru Vijana hao wote warejeshwe katika Makambi ya Kujenga Taifa tayari kwa kuanza mafunzo yao mara moja” amesema Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ)

 

error: Content is protected !!