Samia: Hakuna upungufu wa chakula

HomeKitaifa

Samia: Hakuna upungufu wa chakula

Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado Tanzania ina chakula cha kutosha na hakuna tishio la kuwa na uhaba.

Alibainisha hayo jana katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam wakati akishiriki Jubilei ya miaka 50 ya Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA).

Rais Samia alisema kwenye ghala la hifadhi ya taifa la chakula kuna takribani tani 150,000 kwa ajili ya kutumiwa endapo kutatokea wakati mgumu wa upungufu wa chakula.

Alisema hayo akijibu ombi la Mwenyekiti wa WAWATA, Evelyn Mtenga kuhusu mikakati ya kudhibiti tatizo la njaa nchini kutokana na kuwepo kwa dalili za upungufu wa chakula.

“Mmeliona hili vizuri kwa sababu miaka michache ijayo dunia inaangalia suala la kutokuwa na chakula cha kutosha. Kuna nchi ambazo leo tayari wameshaingia kwenye janga hili na nyingine bado,

“Nataka niwahakikishie Tanzania bado tuko katika hali nzuri pamoja na mavuno hafifu kwa msimu uliopita, ghalani kuna tani zisizopungua 150,000 tumeziweka kwa ajili ya wakati mgumu.” alisisitiza Rais Samia.

 

error: Content is protected !!