Hatua za kuweka chandarua kitandani

HomeElimu

Hatua za kuweka chandarua kitandani

Watu wengi wamekuwa wakishindwa kuweka chandarua (neti) kwa ufasaha na hivyo wakati mwingine hujikuta wakilala na mdudu mbu ndani ya neti.

Kwa kujali na kuthamini afya yako, ClickHabari tunakusogezea hatua unazopaswa kufuata wakati unaweka neti.

1. Tandika kitanda chako vizuri.
2. Shusha chandarua chako huku ukihakikisha upo ndani ili kuona kama mdudu mbu ameingia.
3. Chomeka kila pembe ukiwa ndani ya chandarua.
4. Hakikisha hakuna mbu ndani ya chandarua.
5. Sasa unaweza kulala.

 

error: Content is protected !!