Kizz Daniel azomewa Marekani

HomeBurudani

Kizz Daniel azomewa Marekani

Mwanamuziki kutoka Nigeria, Kizz Daniel amejikuta akizomewa na mashabiki zake nchini Marekani baada ya kuchelewa kwenye tamasha kwa takribani masaa matano bila taarifa.

Mwimbaji huyo anayetamba na ngoma ya ‘Buga’ inayofanya vizuri ulimwenguni, alichelewa kwenye tamasha hilo bila kutoa taarifa wala sababu jambo lililowakasirisha mashabiki zake waliokuwa wakimsubiri.

Hili liliwakasirisha mashabiki zake na kuanza kumzomea huku wakimrushia vitu wakitaka kurejeshewa viingilio vyao.

Ataja sababu ya kuchelewa

Mkali huyo wa ‘Buga’ sasa ameomba radhi  kwa mashabiki wake na akaeleza kuwa alikuwa na tatizo la hati yake ya kusafiria katika Ubalozi mdogo wa Marekani nchini Nigeria na ndiyo sababu hakuweza kuondoka Marekani kwa wakati.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by VADO ‘D GREAT ? (@kizzdaniel)

error: Content is protected !!