Bi Hindu afariki dunia

HomeBurudani

Bi Hindu afariki dunia

Muigizaji na mtangazaji Chuma Selemani maarufu zaidi kama Bi Hindu amefariki Dunia asubuhi ya leo.

Taarifa hii imethibitishwa na Mjukuu wake aliyesema Bi Hindu Amefariki akiwa nyumbani kwake Magomeni

Bi Hindu alikua akisumbuliwa na Maradhi kwa Muda Mrefu Mpaka Umauti ulipomkuta.

Ni mmoja kati ya waanzilishi wa Kundi la Kaole Sanaa na ndiye aliyetoa jina hilo wakati kundi linaanzishwa. Umezoea kumuona akishabikia Klabu ya Simba, ila kihistoria aliwahi kucheza katika klabu hiyo wakati inaitwa Morning Star na Sunderland.
Kwenye uigizaji, Igizo la Gubu la Wifi ndilo lililomfungulia njia. Baadaye alionekana kwenye filamu, ukungwi, UMC kisha utangazaji. Mara ya mwisho alionekana kwenye Tamthiliya ya Maneno ya Kuambiwa.

Bi Hindu enzi za uhai wake

 

error: Content is protected !!