Mambo 5 ya kuepuka kufanya kwa ajili ya Mwanamke

HomeElimu

Mambo 5 ya kuepuka kufanya kwa ajili ya Mwanamke

Kwa kuzingatia historia, mila, tamaduni na desturi, imezoeleka kuwa mara nyingi ni wajibu wa Mwanaume kuonesha upendo kwa mpenzi wake na kujitoa kwa hali na mali kulilinda penzi na mahusiano aliyonayo. Pia ili kuhakikisha Mwanamke ana furaha siku zote Mwanaume hufikia kuchukua uamuzi wa kufanye matendo magumu na yenye kuhatarisha ili tu kumridhisha mpenzi wake. Pamoja na yote katika kufanya hivyo kuwa makini sana usifanye mambo haya 5 kwa mpenzi wako.

1.Usimlipie ada
Utasikia mengi sana, lakini kumbuka mpenzi hasomeshwi na kamwe usije ukathubutu kumlipa ada mpenzi au mchumba wako labda kama ni Mke wa ndoa. Unaweza kumsaidia katika mahitaji madogo madogo lakini sio kumlipia ada labda kama umemuoa na ni mkeo halali.

2. Usifanye uhalifu kwa ajili yake
Kama unaona kwamba hautoweza kutimiza mahitaji yake na huwezi kuendana na maisha yake ni heri ukaachana nae kuliko kwenda kutenda mambo ya kiuhalifu kama kuiba au kupora kwa ajili yake.

3. Usisahau ndoto zako
Kumbuka kabla ya kukutana na mchumba wako ulikua na ndoto zako za maisha hivyo unapokuwa nae usije kusahau kuzitimiza na kuanza kuziishi ndoto zake.

4.Usidharau familia yako
Kuna baadhi ya Wanawake unapokua nao wanakuwa na tabia ya kukushawishi usipende wala kuthamini familia yako, kuwa makini na mtu utakayeamua kuwa naye na endapo utapata wa aina hii kuwa makini usije kuidharau familia yako.

5.Usisahau kujijali
Unapojaribu kutimiza mahitaji yake usije ukajisahau na wewe. Kuna baadhi ya Wanaume wapo tayari walale njaa ila wawatumie wapenzi wao pesa ya kula kuwa makini usiingie kwenye mkumbo huo.

error: Content is protected !!