Wasira awashangaa wanaodai Katiba mpya sasa

HomeKitaifa

Wasira awashangaa wanaodai Katiba mpya sasa

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bunda, mkoani Mara na Mwanasiasa mkongwe nchini, Stephen Wasira akizungumza kwenye kipindi cha medani za siasa kinachorushwa na kituo cha Star Televisheni ameeleza  kwamba kitendo cha Chama cha Siasa nchini (ambacho hakukitaja jina) kutangaza maandamano nchi nzima ni kinashangaza kwani hata nchi zingine hazifanyi maandamano kwa mtindo huo.

“Kuna chama cha siasa ambacho kinaitisha maandamano ya nchi nzima. Mimi nimekaa Marekani wao wanaandamana kwa mambo yao na siyo nchi nzima. Sisi hapa chama kimoja kinasema tufanye maandamano nchini, Mmmnh nchi yote!!! sasa tukiandamana tutalima saa ngapi?” Amehoji Wasira.

Akizungumzia kuhusu madai ya Katiba mpya yanayoendelea, Wasira ameuliza kwamba imekuaje suala hilo limekuwa na umuhimu wakati huo na sio wakati Rais Magufuli alipokuwepo.

“Wapinzani hawakudai katiba mpya wakati wa Rais Magufuli, kwani Katiba imekuwa muhimu leo?  Magufuli aliwajibu kitu gani, walifanyaje kwanini watake sasa hivi tena haraka.” Alihitimisha Mzee Wasira.

error: Content is protected !!