Watayarishaji wa muziki nchini waomba wasanii kuimba nyimbo za kimataifa

HomeKitaifa

Watayarishaji wa muziki nchini waomba wasanii kuimba nyimbo za kimataifa

Baada ya tangazo kuhusu ushirikiano wa chati za muziki za ‘Billboard’ na application ya ‘Boomplay’, watayarishaji wa muziki nchini wamewasihi wasanii kutumia fursa hiyo kutengeneza nyimbo nzuri zitakazoweza kuwepo kwenye chati hizo kubwa zinazotambulika duniani kwani nyimbo zitakazokuwa zinafanya vizuri boomplay zitachukuliwa na kuwekwa kwenye chati za Billboard.

Baadhi ya watayarishaji wa muziki kutoka nchi wamewataka wasanii na waimbaji kuimba nyimbo zenye maana na nzuri ilikuweza kuwekwa kwenye chati hizo kubwa duniani. Mr T Touch ni kati ya watayarishaji wakubwa na wanaofanya vizuri yeye amesema huu ni wakati wa wasanii wetu kufanya mambo makubwa mazuri.

“Huu ni wakati wa wasanii kufanya mambo makubwa mazuri na kutumia vipaji vyao katika uandishi na uimbaji ili kuweza kupata kitu kilicho bora na kuweza kuwa katika chati hizo kubwa.” Amesema T Touch

Pia mtayarishaji mwingine anayefahamika kama Dapro, amesema ni wakati sasa wasanii wakaimba mashairi yenye maana na nyimbo zitakazoweza kutambulika kimataifa pia kuambiana ukweli pindi msanii anapoenda kurekodi nyimbo kwa mtayarishaji yoyote.

error: Content is protected !!