Bibi amwozesha mwanafunzi kwa mahari ya Nguruwe

HomeKitaifa

Bibi amwozesha mwanafunzi kwa mahari ya Nguruwe

Polisi wilayani Nkasi mkoani Rukwa wanamshikilia Kennedy Fumpa mwenye umri wa miaka 37 kwa tuhuma za kuoa mwanafunzi wa darasa la tatu. Kennedy aliozeshwa na bibi wa mwanafunzi huyo kwa mahari ya shilingi 330,000 pamoja na nguruwe mmoja mwenye thamani ya shilingi 70,000.

Taarifa hizo zilipatikana baada ya mwalimu mkuu wa shule aliyekuwa anasoma mwanafunzi huyo kuripoti taarifa za utoro wa mwanafunzi katika ofisi ya serikali ya kijiji, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Godfrey Kalungwizi amesema serikali ya kijiji ilifuatilia na kubaini mtoto huyo amaeolewa na anaishi na mwanaume kama mke na mume.

> Fahamu jinsi Nguruwe wanavyotumika kuimarisha usalama kwenye uwanja wa ndege

Mahari aliyotakiwa kutoa Kennedy ilikua ni shilingi 400,000 lakini alitoa mahari ya shilingi 330,000 pamoja ana nguruwe mwenye thamani ya shilingi 70,000. Mtuhumiwa amekamatwa na kufikishwa polisi na uchunguzi utakapokamilika atapelekwa mahakamani kujibu shitaka hilo.

Mkuu wa wilaya ya Nkasi amesema ni kitu kisichokubalika kumbadilisha mtoto wa kike na nguruwe na sheria ya kumlinda mtoto ipo lazima ifate mkondo wake.

error: Content is protected !!