Fahamu jinsi Nguruwe wanavyotumika kuimarisha usalama kwenye uwanja wa ndege

HomeKimataifa

Fahamu jinsi Nguruwe wanavyotumika kuimarisha usalama kwenye uwanja wa ndege

Nguruwe ni moja ya mnyamaa anayetumika kama kitoweo kwa baadhi ya watu. Kwa miaka mingi nguruwe amekuwa akitumika kama chakula, lakini kutokana na tafiti mbalimbali zinazoendelea duniani, imeonekana nguruwe pia anaweza kutumika kwenye masuala ya usalama, hasa katika viwanja vya ndege.

Viwanja vingi vya ndege vimekuwa vikilima na kuondoa uoto wowote ambao unaweza kuvutia ndege pembezoni mwa viwanja vya ndege, hii yote ni kuzuia ndege kufika eneo hilo na kuweza kusababisha matatizo na kero kwa wasafiri.

Ndege hasa Bata Maji wamekuwa kero kubwa sana katika viwanja vya ndege, pindi warukapo muda mwingine hugongwa na ndege au huingia kwenye injini ya ndege na kusababisha ndege kutua kwa dharura.

Ufumbuzi wa tatizo hilo umepatikana huko Uholanzi ambapo Uwanja wa ndege wa Schiphol umeanza kutumia nguruwe kuondoa tatizo hilo. Kiwanja hicho kimechukua nguruwe 20 na kuwaweka pembezoni mwa uwanja huo ambao awali kulikuwa na mashamba ya viazi vitamu. Bata maji hupenda kuzuri eneo hula kujipatia chakula kwenye mabaki ya mazao hayo.

Kazi kubwa ya Nguruwe ni kula mabaki ya viazi hivyo ili kuondoa uwezekano wa ndege kufika kwenye eneo hilo. Mwaka jana pekee Bata Maji 150 waligongwa na ndege kiwanjani hapo pindi ndege zipaapo au kutua.

Tangu nguruwe waanze kufanya kazi hiyo, hakuna ndege waliofika kwenye eneo hilo. Na kuna teknolojia nyingine zinatumika kuondoa ndege hao, kama muziki pamoja na fataki.

error: Content is protected !!