Rais Samia apanda viwango wanawake 100 wenye ushawishi duniani

HomeKimataifa

Rais Samia apanda viwango wanawake 100 wenye ushawishi duniani

Rais Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa walioorodheshwa katika jarida la Forbes la wanawake wenye uwezo mkubwa duniani 2023 akipanda kutoka nafasi ya 95 hadi 93.

Rais Samia aliyechukua usukani wa kuingoza Tanzania Machi, 2021 kutokana na kifo cha mtangulizi wake Hayati John Magufuli, ameingia kwenye orodha hiyo inayoongozwa na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Benki Kuu ya Ulaya, Christine Lagarde nafasi ya pili.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Rais Samia ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na uwezo wake mkubwa alioonyesha kupitia maagizo ya kukabiliana na changamoto za ugonjwa wa Uviko-19 nchini.

Mbali na namna anavyoendelea kujipambanua katika mapambano dhidi ya Uviko-19 hali iliyoleta ongezeko la watalii nchini kwa kuwa nchi ipo salama, pia ushiriki wake katika diplomasia ya kiuchumi.

error: Content is protected !!