Rais Samia awapongeza watangulizi wake kwa maendeleo

HomeKitaifa

Rais Samia awapongeza watangulizi wake kwa maendeleo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Saluhu Hassan amesema mafaniko ya Tanzania yametokana na maono ya viongozi waliomtangulia.

Rais Samia amesema hayo leo katika maadhimisho ya sherehe za miaka 62 ya Uhuru na Mkutano wa kwanza wa taifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

“Ujenzi wa nchi ni mchakato, hivyo katika kila awamu ya uongozi wa nchi yetu, kuna mchango wa maendeleo ya nchi yaliyofanyika. Mafanikio tuliyonayo leo ni matokeo ya uongozi thabiti, maono na michango ya viongozi walionitangulia.” amesema Rais Samia.

Amewataja viongozi hao kuwa Hayati Mwalimu Nyerere, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamini Mkapa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Hayati John Magufuli.

Amesema kwa maono makubwa ya viongozi hao ndio wamefanikisha taifa kupiga hatua katika sekta mbalimbali.

Aidha, Rais Samia ameahidi kuendeleza mema yote,na kujifunza kutokana na changamoto walizokutana nazo viongozi hao.

“Maono na ushupavu mkubwa katika uongozi wao (watangulizi wake) ndio matunda tunayoyafaidi leo hii. Ahadi yangu ni kuyaendeleza mema yote yaliyoiletea nchi yetu maendeleo na kujifunza kutokana na changamoto walizokutana nazo.” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!