Kiswahili chatambulika rasmi kama lugha ya kazi Umoja wa Nchi za Afrika (AU)

HomeKitaifa

Kiswahili chatambulika rasmi kama lugha ya kazi Umoja wa Nchi za Afrika (AU)

Mkutano wa 35 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) umeridhia na kupitisha ombi la Tanzania la kutaka Kiswahili kiwe lugha ya kazi katika umoja huo. Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango aliwasilisha ombi hilo katika mkutano huo.

Dk Mpango alisema Kiswahili ni miongoni mwa lugha za kiafrika zenye wazungumzaji wengi barani Afrika na nje ya bara hilo, pia Kiswahili kinatumika katika jumuiya mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufundishwa shuleni katika nchi nyingi za Afrika.

Sambamba hayo Kiswahili kimepata mafanikio zaidi katika siku za karibuni ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitangaza tarehe 7, Julai kuwa siku ya maadhimisho ya lugha ya Kiswahili duniani lakini pia ulichagua Tanzania kuwa mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU).

error: Content is protected !!