Serikali kufanya tathmini kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na vinywaji

HomeKitaifa

Serikali kufanya tathmini kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na vinywaji

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji akiwa jijini Dodoma jana alitoa taarifa inayoelezea tathmini ya mwenendo wa uzalishaji, usambazaji na bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu. Kutokanaa na Tathmini hiyo Serikali imewaagiza wazalishaji, wasambazaji na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi na vinywaji baridi washushe bei za bidhaa hizo mara moja.

Hii ni baada ya kuwepo malalamiko kuhusu upandaji holela wa bei ya bidhaa hasa vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine yakiwemo mafuta ya kula, sukari na uhaba wa vinywaji baridi.Sambamba na hilo mamlaka husika zimetakiwa kuchukua hatua kali kwa wote watakaobainika kupanga bei kubwa za bidhaa hizo kwa kuwa wanahujumu uchumi.

“Tathmini inaonyesha kuwa ongezeko holela la bei za vifaa vya ujenzi, hususani saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa hizo ambapo kuna mnyororo mrefu wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.” alisema Dk. Kijaji

Dk. Kijaji alisema gharama halisi za uzalishaji wa saruji haiakisiwi katika bei ya saruji iliyopo sokoni ikilinganishwa na uwiano huo katika nchi jirani na kwingineko duniani, Ongezeko la bei ya saruji halina uwiano halisi na gharama za usafirishaji na usambazaji nba pia haina uhusiano na mwenendo wa nguvu za utashi wa mlaji na ugavi.

 

error: Content is protected !!