Mpoto alamba shavu Wizara ya Maji

HomeKitaifa

Mpoto alamba shavu Wizara ya Maji

Msanii nguli wa kughani mashairi na muziki Mrisho Mpoto amelamba shavu katika Wizara ya Maji baada ya kuteuliwa na Waziri wa Maji, Jumanne Aweso kuwa Balozi wa Sekta ya Maji.

Taarifa za uteuzi huo zimetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Florence Temba kuwa Mpoto atakuwa akiitangaza sekta hiyo kupitia kazi zake za sanaa katika shuguli mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali.

“Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo kuimba wimbo wenye maudhui bora na kusheheni takwimu sahihi kuhusu sekta ya maji katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Bunda, mkoani Mara,” alisema Florence.

Mrisho Mpoto ni mmoja kati ya wasanii bora wa muziki katika Ukanda wa Afrika Mashariki, aliyebobea katika kutumia vionjo vya kiasili kufikisha ujumbe kwa hadhira.

 

error: Content is protected !!