Keisha alilia mrabaha wake bungeni

HomeKitaifa

Keisha alilia mrabaha wake bungeni

Msanii na Mbunge wa Viti Maalumu Khadija Taya maarufu kama Keisha, amefunguka bungeni na kuanza kudai mirabaha na kusema na yeye anastahili kupewa kwani nyimbo zake zinapigwa sehemu mbalimbali.

“Yote hayo ni mambo mema, lakini ninachotaka mfahamu ninyi Wizara ni kuwa mimi sijapewa mrabaha wangu wakati kila mmoja anajua kuwa nyimbo zangu zinapigwa kila mahali hapa nchini, lakini mmefanya vizuri kuanza kutoa najua nitapata,” alisema Keisha.

Aidha , Keisha alitoa pongezi kwa Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu kwakuwa sikivu na kutekeleza kwa wakati changamoto zinazotolewa na kusema kwamba zoezi hili la ugawaji wa mirabaha litachochea ubunifu na utendaji kazi zaidi kwa wasanii.

Hivi karibuni Serikali kupitia Taasisi ya Hati Miliki Tanzania (COSOTA), imeanza kugawa pesa za mirahaba kwa wasanii kutokana na kazi za wanazofanya huku baadhi ya wasanii waliopokea fedha hizo ni Ali Kiba, Rose Muhando, Nandy, AY na Christina Shusho.

 

error: Content is protected !!