Anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuchunguzwa

HomeKitaifa

Anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuchunguzwa

Kaminshna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamisi, amesema wanamchunguza askari wao anayetuhumiwa kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja (ushoga) na ikithibitika, atafukuzwa kazi na kushtakiwa mahakamani.

Kutokama na mkasa huo, Kamishna Hamad alisema ofisi yake ina mpango maalum wa kuwasaka askari wake wote wenye hulka na kujihusisha na matendo ya aina hiyo.

“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kadhia na hiyo ikiwamo kufanyiwa kipimo askari huyo ili kujidhihirisha kama kweli anafanya kitendo hicho… ingawa tumeona video katika mitandao ya kijamii lakini hatuwezi kusema moja kwa moja kama ni kweli au sio kweli,” alifafanua.

Kamishna Hamad alisema askari anapokuwa shoga, hukosa uaminifu na ukakamavu katika jukumu lake la msingi la kulinda raia na mali zao.

“Huu sio utamaduni wa Jeshi la Polisi na wala hakutumwa hivyo. Matendo ya mtu binafsi lazima yatafautishwe na taasisi.

“Hata hizo picha zinazosambaa hazionyeshi kuwa amevaa sare za polisi au kufanya kitendo hicho kwenye kituo cha polisi, hivyo isitafisiriwe kuwa Jeshi la Polisi ndio limefanya.”

Aidha, Kamishna Hamad aliwataka askari wote wenye mwenendo wa aina hiyo wajisalimishe kwenye uongozi ili warekebishwe waendane na utamaduni wa jeshi hilo.

error: Content is protected !!