Sababu ya maduka ya Game kufungwa

HomeKitaifa

Sababu ya maduka ya Game kufungwa

Kampuni ya Massmart kutoka Afrika Kusini inayomiliki maduka ya Game imetangaza kuwa Disemba 25, 2022 ni mwisho wa maduka yake kutoa huduma Tanzania.

Massmart imefikia hatua hiyo ikiwa ni miezi 12 ya kujaribu kuuza maduka hayo nchini Nigeria, Ghana, Tanzania, Kenya na Uganda kwa wawekezaji wapya wa ndani bila mafanikio.

“Tunatarajia siku ya mwisho ya kufanya biashara maduka yetu ya Game kwenye nchi za Afrika Mashariki na Magharibi (Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana na Nigeria), itakuwa Desemba 25.’’ imesema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, kuhusu hatua ya kufunga maduka yao nchini na barani Afrika kwa ujumla.

Kampuni hiyo inasema kwa sasa wako kwenye hatua za haraka kuanza uuzaji wa jumla wa bidhaa zilizopo katika maduka yote kwenye nchi husika.

error: Content is protected !!