Kanye West aja na style mpya ya nywele

HomeBurudani

Kanye West aja na style mpya ya nywele

Rapa kutoka nchini Marekani, Kanye West ameamua kuja na muonekano mpya wa kunyoa nywele zake ambao umewaacha hoi mashabiki wengi huku watu wengine hapa Tanzania wakiubatiza kwa jina la ‘Mpunyuo style’.

Kanye West aliweka picha kwenye ukuarasa wake wa Instagram ikimuonesha akiwa kwenye muonekano huo bila kuandika chochote. Kanye anatajwa kama miongoni wa wabunifu wenye ushawishi mkubwa duniani kwa sababu kila mara anakuja na vitu vipya ambavyo vinafanikiwa kuliteka soko.

Mbali na aina ya unyoaji aliokuja nao Kanye anamiliki biashara ya kutengeneza viatu ambayo viatu vyake mara nyingi vimekua vinashangaza watu lakini pia anamiliki ‘Kanisa’ ambalo halina sheria, lakini wanamsifu Mungu kupitia nyimbo za kidunia zilizobadilishwa maneneo na kuwekwa ujumbe wa Mungu.

error: Content is protected !!