Serikali yatoa msamaha wa kodi matrekta kutoka nje

HomeKitaifa

Serikali yatoa msamaha wa kodi matrekta kutoka nje

Sekta ya kilimo nchini imepata misamaha ya kodi katika eneo la kuagiza matrekta nje ya nchi lengo likiwa ni kusaidia kilimo nchini.

Ofisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya, Nicodemus Massawe alisema hayo katika Maonesho ya Kilimo yanayoendelea katika Viwanja vya Mwakangale mkoani Mbeya.

Massawe alisema matrekta, vitalu, nyumba, mbolea na pembejeo zinazohusu kilimo yanapoingia nchini yana msamaha wa kodi kwa kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa.

“Kwa hiyo wakulima wadogo, wa kati na wakaubwa watutembelee hapa Nanenae ili wajue ni vitu gani vimesamehewa na gharama zake zilizosamehewa ni kiasi gani ili anapoagiza hizo zana kwa ajili ya kuboresha kilimo iwe rahisi kwake na mwisho wa siku kilimo kiwe na tija,” alisema.

Alisema kwenye sheria ya kodi ya mapato imewekwa katika makundi mawili, mkulima na anayelima kibiashara anatakiwa kulipa kodi ya mapato.

Aidha alisema sheria inamtambua mkulima huyo kwa kuangalia thamani ya mavuno yake kama inaanzia Sh milioni nne anapaswa kulipa kodi, ikishuka hapo inakuwa ni mkulima wa kilimo cha kujikimu.

 

error: Content is protected !!