Tanzania yashika nafasi ya pili utalii Afrika

HomeKimataifa

Tanzania yashika nafasi ya pili utalii Afrika

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Hassan Abbas, amesema Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kupata watalii wengi zaidi Afrika kwa robo ya kwanza ya mwaka kuanzia January hadi Machi,2023.

Kwa kipindi hicho Tanzania ilipata watalii zaidi ya 800,000, ikilinganishwa na watalii 200,000 kwa mwaka 2022 kwa kipindi hicho cha robo mwaka, ambapo nchi ya kwanza ni Ethiopia na ya tatu ni Morocco.

Akizungumza Dar es Salaam leo, wakati akieleza mafanikio ya mkutano wa 66 wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO), Kamisheni ya Afrika uliofanyika Mauritius kuanzia Juni 26, amesema mafanikio mengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengera kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais.

“Kwa mara ya kwanza tangu kujiunga na UNWTO, tumepata nafasi ya juu ya uongozi katika mkutano huo, ambapo waziri ataiwakilisha bara la Afrika katika mikutano ya UNWTO kupitia nafasi hiyo tutatangaza vivutio vyetu vya utalii duniani kupitia matukio na mikutano itakayoandaliwa na UNWTO,” ameeleza.

error: Content is protected !!