Mradi wa Kawe Beach mbioni kuanza baada ya kusitishwa kwa miaka 7

HomeKitaifa

Mradi wa Kawe Beach mbioni kuanza baada ya kusitishwa kwa miaka 7

Mradi mkubwa wa mali isiyohamishika maarufu kama Seven-Eleven (711) ulioko katika eneo la Mbezi Beach/Kawe roundabout jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuendelea kujengwa baada ya kusitishwa kwa miaka mingi.

Mradi wa nyumba za makazi wa 711 ambao ulipaswa kukamilika ndani ya miaka mitatu ulisitishwa kwa muda wa miaka saba tangu utawala wa serikali uliopita.

Akizungumza na wahariri jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bwana Hamad Abdallah, alisema mazungumzo yanaendelea na ujenzi utaanza tena mwezi wa Septemba huku asilimia 85 ya apartimenti tayari zimeuzwa kwa wapangaji licha ya kutokuwa tayari kwa kukamilika kwa mradi.

Aidha aliweka wazi kwamba NHC, ambayo ni taasisi ya serikali, na wamiliki wa mradi huu wa mali isiyohamishika wenye thamani ya Shilingi bilioni 105 wamepata hasara kubwa tangu mradi huu uliposimamishwa.

 

error: Content is protected !!